Showing posts with label NEWS (HABARI). Show all posts
Showing posts with label NEWS (HABARI). Show all posts

MASWALI TATA KUHUSU UGONJWA WA DENGUE

Dar es Salaam.Tangu ugonjwa wa homa ya  dengue uibuke mkoani Dar es Salaam na baadaye maeneo mengine ya nchi, wananchi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi yenye utata ambayo sasa yamepata majibu ya wataalamu.

1. Kwa nini mbu wengine wakiwamo wanaoambukiza malaria hawawezi kuambukiza dengue?Mtafiti wa tabia za mbu kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), Dk Nicholaus Govela alisema mbu anayeambukiza homa ya dengue, Aedes Egypti, hawezi kubeba vimelea vya malaria wala yule anayeambukiza malaria hawezi kuambukiza dengue kutokana na maumbile yao.

Dk Govela alisema fiziolojia ya mwili wa mbu haiwezi kuruhusu Aedes Egypti kubeba virusi vya mbu mwingine.“Ndiyo maana mbu hawezi kuambukiza Virusi vya Ukimwi,” alisema.

2. Kwa nini mbu wa dengue huuma mchana?Dk Govela alisema suala hilo bado linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kati ya aina tatu za mbu wanaosababisha dengue, hakuna utafiti uliofanyika kujua tabia zao wote.
Aina hizo ni Aedes Egypti, Aedes Albokictus na Aedes Africaans.Alibainisha kuwa katika tafiti zinazofanyika, IHI iliwahi kubainika kuwa Aedes African ambaye pia anaambukiza dengue huuma usiku.

Alisema wengi wanamwelezea mbuhuyu kwa kumlinganisha na tabia zambu wa Japan, China na America yaKusini lakini inawezekana huyu aliyepo hapa ni mpya tofauti na wa nchi za nje.

3. Je, dawa inayopulizwa inafaa kuwaangamiza?Dk Govela alisema inawezekana ndiyo au hapana, lazima hili pia lifanyiwe utafiti kwa kuwa upo uwezekano wa mbu hawa kujenga usugu wa dawa kwa kuwa wamekuwapo nchini kwa miaka mingi.
Alipongeza uamuzi wa Serikali wa kupuliza dawa kwenye mabasi ya mikoani lakini bado alihoji iwapo imefikiria udhibiti kuanzia katika viwanja vya ndege na iwapo itawezekana kuzuia watu wanaokwenda mikoani wakiwa tayari wameambukizwa.

4. Je, kuna watu wanaougua dengue bila kuonyesha dalili?Mtafiti huyo alisema wapo wanaougua bila kuonyesha dalili na wanaendelea kuambukiza... “Hawa mara nyingi hawaendi hospitali lakini wanakuwa na virusi mwilini,” alisema.

5. Kuna aina ngapi za virusi vya dengue?Dk Govela alisema zipo aina nne zavirusi vinavyoambukiza dengue.
Alivitaja kuwa ni;
den 1,
den 2,
den 3
na den 4.
Hadi sasa, wanasayansi hawajaweza kubaini ni virusi vya aina gani vinasababisha homa hiyo kwa Tanzania.“Ndiyo maana tunahitaji kufanya tafiti zaidi,” alisema.

6. Je, juisi ya majani ya papai ni tiba ya dengue?Ofisa wa Taaluma na Udhibiti wa Magonjwa wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Grace Saguti alisema haijathibitishwa kisayansi.Dk Saguti alisema ili tiba ikubalike, lazima ithibitishwe na hakuna namna mbadala ya kuiruhusu itumike kabla ya kujua madhara na faida zake.

Alisema mpapai unaongeza vitamini A na hivyo kuimarisha kinga ya mwili, lakini si kutibu virusi vya dengue ambavyo kwa asili yake havina dawa.

7.Mbu wa dengue wako Dar es Salaam pekee?Mtaalamu wa IHI alisema mbu huyo anaishi katika maeneo ya kitropiki, hivyo huenda yupo hata katika mikoa mingine.

Alisema kwatabia, aedes africans anafanana na mbu aina ya culex ambaye anapatikana katika mikoa mingine, hivyo hata huyo anaweza kuwapo huko pia... “Lazima ufanyike utafiti ili tujue iwapo mbu huyo hawezi kuzaliana katika mikoa mingine,” alisema.

8. Kwa nini aedes hupenda maji masafi yaliyotuama?Dk Govela alisema ni kutokana na asili ya maumbile yao. Mbu hao huamini maji masafi yaliyotuama huwapa joto zaidi kwa ajili ya kutaga mayai.“Lakini si lazima wawe wanazaliana zaidi katika maji masafi kwa sababuwana tabia ya kubadili tabia.

Kwa mfano, anopheles wanaoeneza malaria nao walipenda maji masafi awali, lakini kwa sasa wamebadilikawanazaliana hata kwenye maji machafu,” alisema

9.Kwa nini wahudumu wa afya wanaathirika zaidi?Daktari Kiongozi na Mtaalamu wa Homa ya dengue, Mrisho Lupinda alisema nao ni binadamu kama wengine na wanaishi maeneo hatarishi yenye mbu kama watu wengine.

10. Kwa nini panadol pekee ndiyo inatibu dalili za dengue?Dk Lupinda alisema dawa nyingine za maumivu yaani Diclopar, Diclofenac na Aspirini huingiliana na mfumo wa chembe hai nyeupe za damu na huweza kusababisha chembe hizo kupungua mwilini.

Dawa hizo huchochea kutengeneza sumu ambayo huathiri baadhi ya ogani za mwili.Ugonjwa wasambaaHoma ya dengue imesambaa katikamaeneo mbalimbali nchini na kutoka Shinyanga, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Fredrick Mlekwa amesema kumetokea kifo cha mtoto aliyekuwa na dalili zote za ugonjwa huo.

Huko Arusha, mkazi wa Maji ya Chai, Frank Nnko (30) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akitokea Hospitali ya Wilaya ya Meru akiwa na dalili za homa hiyo.

Zanzibar, wagonjwa watatu wanaodhaniwa kuwa na homa ya dengue wamelazwa katika HospitaliKuu ya Mnazi Mmoja. Waziri wa Afya, Juma Duni Haji alisema wagonjwa hao wana dalili za ugonjwa huo.

Mtu mmoja amelazwa katika Hospitali ya Tumbi akiwa na dalili za dengue, akiwa na maumivu ya kichwa na kutoka damu puani, Ofisa Habari wa Hospitali hiyo, Gerald Chami alisema mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 30, alitokea Mbezi Wilaya ya Kinondoni.Imeandikwa na Florence Majani, Andrew Msechu, Stella Ibengwe na Happy Lazaro, Mwinyi Sadallah, Talib Ussi na Julieth Ngarabali.

W.H.O(World Health Organization) YAJITOSA DHIDI YA UGONJWA WA DENGUE


Dar es Salaam.


Shirika la Afya Duniani (WHO), limejiunga katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa ya dengue kwa kuagiza vipimo 1,000 kwa ajili ya upimaji nchi nzima.


WHO imechukua hatua hiyo kusaidia juhudi zinazoendelea za kupambana na homa hiyo na imeagiza utafiti zaidi ufanyike ili kutambua aina halisi ya virusi vya dengue vilivyopo nchini kwa kulinganisha na vile vinavyopatikana katika maeneo mengine duniani.


Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa wa Taaluma na Udhibiti wa Magonjwa wa WHO, Dk Grace Saguti alisema tayari chombo hicho kimeagiza vipimo hivyo vitakavyo gharimu Sh17.7 milioni na kila kimoja kinaweza kupima sampuli 25, hivyo kunufaisha watu 25,000.


Hatua hiyo imechukuliwa huku kukiwa na taarifa kwamba baadhi ya hospitali za Serikali za wilaya na rufaa zinakabiliwa na uhaba wa vipimo, hali iliyosababisha kutoza kati ya Sh25,000 hadi Sh30,000 kwaajili ya kupima mgonjwa mmoja.


Katika vituo binafsi, wagonjwa wamekuwa wakipimwa kwa gharama inayofikia Sh50,000 hadi 60,000 kwa kila mtu.Juhudi hizo za WHO zimetangazwa siku moja baada ya Serikali kupitia Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk Steven Kebwe kulieleza Bunge kuwa kwa sasa vipo vipimo 350 na Serikali inatarajia kuagiza vingine 750.


Dk Saguti alisema WHO imeshatengeneza miongozo, mikakati na mafunzo pamoja na kutoa vitendea kazi ili kujua namnaya upimaji na udhibiti."Sheria za afya za kimataifa za mwaka 2005 hadi 2007, zinaelekeza nchi kuhusu tatizo lolote lisilo la kawaida liripotiwe WHO.


Serikali ya Tanzania ilifanya hivyo na miongozo ya homa ya dengue ikatolewa," alisema.Alisema miongozo iliyotolewa na WHO ni pamoja na tatizo la dengue lisiachwe mikononi mwa Wizara ya Afya pekee, bali sekta zote zihusishwe katika kuudhibiti.Miongozo mingine ni uhamasishaji wa upatikanaji wa vipimo ili kuhakikisha watu wenye dalili hizo na ambao wamepimwa hawana malaria, wanapimwa na kutibiwa kama inavyotakiwa.


Alisema miongozo mingine ya WHO ni kuwapo rasilimali fedha ili vituo vya afya viwe na dawa pamojana vipimo.Tayari Rais Jakaya Kikwete ameagiza Wizara ya Fedha na ile ya Afya kushirikiana na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kupambana na ugonjwa huo kwa dharura.


Takwimu..


Jambo lingine ambalo WHO imeishauri Serikali ni kutafuta takwimu sahihi ili kujua ukubwa wa tatizo na kulifanyia kazikulingana na uzito wake."Uhakiki wa takwimu, ushahidi na taarifa sahihi za magonjwa ni suala muhimu katika kudhibiti.


Ndiyo maana tunaitaka wizara kuhakikishainapata takwimu sahihi," alisema. Alisema wizara hiyo inatakiwa iwe na mfumo mzuri wa takwimu kuanzia ngazi yachini na ihusishe sekta za Serikali na zile binafsi.


Wakati hadi jana takwimu za Serikali zilionyesha kuwa idadi ya watu waliougua wamefikia 460, takwimu zilizopatikana katika baadhi ya hospitali jijini Dar es Salaam zilionyesha kuwa walikuwa wamefikia 677, achilia mbali waliokuwa wameugua kati ya Oktoba mwaka jana hadi Machi.


Katika uchunguzi huo wa gazeti hili,ilibainika kuwa Mwananyamala wamefikia wagonjwa 142, Amana (54), Maabara ya Lancet (53), Hindul Mandal (26), Aga Khan (11), Kliniki ya IST (245), Regency (63), Temeke (15), Dk Mvungi (3) Muhimbili (65).


MSD: Tuna vipimo vya kutoshaWakati baadhi ya hospitali zikiripotiuhaba wa vipimo, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifani amesema inavyo vya kutosheleza mahitaji."Sisi wakati wote tupo tayari kupambana na dharura, si tukwa sababu ya mlipuko, pia hatuhusiki kabisa na masuala ya kuongezeka kwa bei za vifaatiba audawa hospitalini kwa sababu ni taasisi ya Serikali," alisema. Mmojawa wasambazaji wa vipimo vya upimaji wa dengue,


Ally Hamimu alipiga simu chumba cha habari jana na kueleza wasiwasi wake kuhusu gharama za vipimo kuwa akisema ni kubwa kuliko uhalisia.??


Tunaamini kuna vipimo mbalimbali vya kupima homa ya dengue lakini hata kama hospitali zinatafuta faida, zinatakiwa kutoza kati ya Sh13,000 na Sh15, 000 kwa kipimo," alisema Hamimu na kutolea mfano vitendanishi vya Dial Lab Dengue lgG/lgM ambavyo boksi la vipimo 30 huuzwa kati ya Sh175,000 na Sh190,000."


Hii inamaanisha kuwa kipimo kimoja kwa rejareja kinaweza kuuzwa kati ya Sh6,500 hadi Sh7,500 na huduma za kupima zisizozidi Sh15,000. "Sasa kutokana na mahitaji kuwa makubwa ya vipimo hivi baada ya mlipuko wa dengue, baadhi ya wamiliki wa hospitali wanapandishabei, wananchi wasikubali," aliongeza Hamim.


Dk Buberwa azikwa Wakati huohuo, mamia ya wakazi wa Dar es Salaamwakiwamo madaktari na watumishiwa hospitali mbalimbali, jana walijitokeza katika Makaburi ya Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam kumzika Dk Gilbert Buberwa aliyefariki dunia Jumapili kutokana na homa ya dengue.


Dk Buberwa aliyekuwa daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya akili katika Hospitali ya Temeke, ameacha mke na watoto wawili.Andrew Msechu, Florence Majani, Nuzulack Dausen na Julius Mathias

SERIKALI YATENGA Sh. Mil. 500 KUUKABILI UGONJWA WA DENGUE

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetenga shilingi milioni 500 kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya "Dengue" ambao umesababisha vifo vya watu watatu kuanzia Januari mpaka mwezi huu.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Kebwe Stephen Kebwe amesema tangu ugonjwa huo ugundulike nchini, wagonjwa waliothibishwa kuugua ugonjwa huo ni 450 na kati ya hao wagonjwa wapya 60 wamegundulika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.Pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali za kupambana na ugonjwa huo kama kutoa elimu kwa wananchi, Timu ya Taifa ya maafa kukutana mara mbili kwa wiki ili kutathimini mikakati ya dharura, Naibu waziri huyo amewataka Watanzania kutokuwa na hofu kwani maambukizwi ya ugonjwa huo hayatokani na kumhudumia mgonjwa au kumgusa.Katika hatua nyingine Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dokta Hussein Mwinyi amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2014/2015.Amewahakikishia watanzania hali ya usalama nchini kuwa ni shwari licha ya kuwepo kwa matishio na mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Msemaji kutoka kambi ya Upinzani kwa wizara hiyo Masoud Abdallah Salim yeye ameitaka Serikali kuwakumbuka na kuwathamini wanajeshi wastaafu.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ili iweze kutekeleza majukumu yake imeidhinishiwa shilingi trilioni 1.2 ilizozitenga katika bajeti ya mwaka 2014/2015.
Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 249 zitatumika katika miradi ya maendeleo.

MTOTO WA MIEZI SITA ASHITAKIWA MAHAKAMANI

A nine-month-old boy charged with planning a murder, threatening police and interfering with state affairs in Pakistan has been grantedbail after appearing in court this week.
Toddler Muhammad Mosa Khan wasbooked in February along with 30 other people, including a number of members of his family, after stones were allegedly thrown at police and energy officials during raids on homes in Lahore.

Residents had been accused of not paying for electricity.Apparently deciding that the nine month old was capable of - and had - taken part in the alleged stone throwing, Sub-Inspector Kashif Ahmed decided to arrest the child.What followed were farcical scenes in which the toddler was fingerprinted and made to sit on his grandfather’s lap in court, drinking his bottle.

The judge quickly granted bail for the child, along with the other people accused in the case. Baby Muhammad is however currently expected back in court on 12 April -although the judge apparently noted the absurd nature of the charge, he does not have the powers to dismiss the case against.

RAIS KIKWETE APEWA TUZO YA UONGOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika katika sherehe kubwa iliyofanyika Washington nchini Marekani.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania Tuzo hiyo ambayo imepokelewa, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine kwa Rais Kikwete kwa kuwa "Kiongozi wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013."Pamoja na Rais Kikwete, Waafrika wengine ambao wamepewa heshima kwenye sherehe hiyo ni Dkt. Kingsley Moghalu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria na Bwana John Kennedy Opara, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mahujaji Wakristo wa Nigeria ambaye pia ni mshauri wa Rais Gooluck Jonathan wa nchi hiyo kuhusu mahusiano ya kidini nchini Nigeria.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Bwana Benard Membe, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Balozi wa Nigeria katika Marekani, Profesa Ade Adefuye ambaye naye amepokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Jonathan ambaye, kama alivyo Rais Kikwete, hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo.Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington nchini Marekani, lilimchagua Rais Kikwete kushinda Tuzo hiyo kwa mwaka 2013 baada ya wasomaji na wadau wake wengine wa Jarida hilo kuwa wamemchagua kwa njiaya kura ya maoni Rais Kikwete kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika.

Tuzo kama hiyo ilitolewa mwaka 2012 kwa Rais wa Sierra, Mheshimiwa Ernest Bai Koroma, ambaye naye alishinda Tuzo hiyo mwaka huo.Akizungumza kabla ya kukabidhi Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Membe, Balozi Adefuye wa Nigeria katika Marekani amemwelezea kwa undani anavyomfahamu Rais Kikwete akisisitiza kuwa kiongozi huyo wa Tanzania ni kielelezo cha rika jipya la viongozi wa Afrika ambao dira na visheni yao ni maendeleoya Bara la Afrika na wananchi wake.Aidha, akizungumza katika hotuba yake ya utangulizi mwanzoni wa sherehe hiyo, Mchapishaji wa Jarida la African Leadership Magazine, Dkt. Ken Giami ameeleza jinsi Rais Kikwete alivyochaguliwa kwa kishindo na wasomaji na wadau wengine wa Jarida hiyo kutokana na mafanikio yake katika uendeshaji na utawala bora wa Tanzania pamoja na mafanikio yake katika ustawi wa kiuchumi wa wananchi wa Tanzania.

WATOTO WABOBEA KATIKA ULEVI HUKO ULAYA

Sasa tatizo la ulevi lawavamia watoto chini ya umri wa miaka 10 chini Uingereza huku wengine wakilazwa hospitalini.Wataalam wanasema karibu watoto wapatao 380 wamefikishwa hispitalini na kulazwa kutokana na kuchanganyikiwa kuliko sababishwa na ulevi.Kunywa pombe Uzeeni ni hatari kwa akili . mzee huanza kuwa na matatizo ya kusahau sahau na kuonekana mkosa hekima na busara.Wataalam wagundua kuwa muziki mwaafaka ni mtamu hata zaidi yastarehe ya ngono...Muziki unamaliza uasherati.

OPRA WINFREY APATA HAKI KUONYESHA FILAMU YA MANDELA..


Oprah akiwa katika pozi la picha na Hayati Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake....          


Los Angeles, Marekani. Mwanamama mwenye ushawishi Duniani Opra Winfrey, kupitia Kituo chake cha runinga cha ‘OWN’, amepata haki ya kuonyesha filamu ya marehemu Mandela iitwayo ‘Long Walk to Freedom’.
Filamu hiyo imeshapata umaarufu mkubwa na kutajwa kuwania tuzo kadhaa. Itakuwa inaeleza maisha halisi ya mwanamapinduzi huyo.
Kwa mujibu wa waandaaji wa filamu hiyo, itachukua miaka mitatu kabla ya kuanza kuonyeshwa kwenye runinga na itakapoanza kituo cha kwanza kuionyesha kitakuwa ni ‘OWN’ ambacho kimenunua haki hizo kutoka kwenye Kampuni ya ‘The Weinstein’.

Miongoni mwa watu waliowahi kumfanyia mahojiano yaliyojaa kila aina ya ushujaa, vilio hayati Nelson Mandela ni mtangazaji Opra ambaye alihudhuria mazishi ya mwanamapinduzi huyo jasiri Kijijini cha Qunu, alikozaliwa Mandela.

MASHEIKH WASISITIZA UMOJA NA AMANI...

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik (kulia), wakiwa kwenye sherehe za Maulid kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam juzi usiku.

 Kwa ufupi
“Ninaomba Waislamu na watu wa dini nyingine kuwa pamoja, tuondoe tofauti zetu kwani sisi Watanzania ni watu tuliozoeleka kwa kuwa na amani, nisingependa kuona dini zetu zinasababisha uvunjifu wa amani.”

Dar es Salaam/Mikoani. Viongozi mbalimbali wa siasa na Kiislamu nchini, wamehimiza amani, umoja, mshikamano wa Watanzania ili kuliepusha taifa na balaa la kupoteza amani.
Walisema hayo katika maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika juzi usiku.
Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi aliwataka watu wa dini zote kuondoa tofauti zao ili kudumisha amani iliyopo nchini kwa muda mrefu na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba amewataka Waislamu nchini kuepuka migogoro ndani ya misikiti inayoweza kuwagawa.
Mufti
Akihutubia mhadhara wa kitaifa wa Waislamu uliofanyika kwenye Viwanja vya Stendi ya Ujiji, Kigoma, Mufti Simba aliwataka waumini wa dini hiyo kuepuka migogoro ndani ya misikiti inayoweza kuwagawa na kuzusha vurugu miongoni mwao.
Alisema migogoro na vurugu ndani ya misikiti imesababisha Waislamu kukosa nguvu na umoja miongoni mwao na kujikuta wakipoteza fursa ya kupiga hatua za maendeleo kwa kujenga miundombinu ya kijamii kama vile shule, vyuo vikuu na hospitali.
“Ninawaasa Waislamu kuwa makini na baadhi ya watu wanaotaka kutugawa kwa masilahi yao binafsi. Tuepuke sana migogoro baina yetu ndani ya misikiti, wale wanaouza viwanja vya misikiti na mali za Waislamu hawana budi kuacha mambo hayo mara moja kwa vile ndiyo kiini cha migogoro mingi.
“Tujifunze kwa wenzetu Wakristo ambao kila wanapopata viwanja, huvitumia kujenga miundombinu ya shule, vyuo na hospitali ambazo mwishowe zinatusaidia hata sisi Waislamu kupata maarifa. Hapa ndipo tunapotakiwa tujifunze kufanya mema ndani ya jamii zetu kwa faida ya taifa na Waislamu wenzetu.”
Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Hamid Jongo aliwataka Waislamu kuacha kulalamika kwamba Serikali inawakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo akisema jambo hilo si kweli.
“Waislamu tumekuwa tukilalamika kwamba kuna mfumo-kristo unaofanya kazi ndani ya Serikali na utawala wa nchi yetu. Hizi tuhuma si za kweli na hazipo kabisa. Zaidi kinachotugharimu sisi Waislamu ni kuendekeza migogoro baina yetu na kufanya mambo yasiyo ya kistaarabu katika Jamii,” alisema Sheikh Jongo.
Alisema baadhi ya kesi zilizopo mahakamani zilizofunguliwa na Waislamu dhidi ya wenzao ni dalili ya kushuka kwa maadili na hivyo kuwa kichocheo cha kudumaza maendeleo ya Waislamu.

Pia alitaja ugomvi unaotokea ndani ya misikiti kuwa ni miongoni mwa mambo yasiyokubalika katika jamii ya Kiislamu.
Mwinyi
Akizungumza kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Rais huyo Mstaafu alisema ili kudumisha umoja wa muda mrefu wa Watanzania, ni vyema watu wa dini zote wakashirikiana katika kila jambo ili kuimarisha mshikamano. “Ni vizuri kwa Watanzania wa dini zote nchini kuondoa tofauti zao na kujenga umoja na mshikamano ili kudumisha amani. Tumeshuhudia matukio mbalimbali yanayohusishwa na masuala ya kidini kama; uchomaji moto wa makanisa yalitotokea Visiwani Zanzibar na Bara, umwagiaji wa tindikali kwa viongozi wa dini...”
Akizungumza kwa hisia, Mzee Mwinyi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kuwa wamoja licha ya kuwa kila mtu ana dini yake... “Ninaomba Waislamu na watu wa dini nyingine kuwa pamoja, tuondoe tofauti zetu kwani sisi Watanzania ni watu tuliozoeleka kwa kuwa na amani, nisingependa kuona dini zetu zinasababisha uvunjifu wa amani.”
“Mwenyezi Mungu hatukatazi, kushirikiana pamoja hivyo kwa hiyo tushirikiane, tupendane na tuimarishe umoja wetu ambao ndiyo sifa kubwa tuliyokuwa nayo kwa muda mrefu.”
Lindi
Akihutubia katika Maulid yaliyofanyika kimkoa kwenye Uwanja wa Ilulu Mjini Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk Nassor Hamid alisema ni wajibu wa jamii kutambua kuwa amani na utulivu wa nchi umetokana na umoja na mshikamano uliojengwa ambao hautakiwi kuchezewa na mtu, kikundi, taasisi wala vyama vya siasa.
Dk Hamid aliwataka viongozi wa dini zote kutoa elimu ya maadili kwa waumini wao ili kuepuka mmomonyoko wa maadili kwa jamii.
Alisema kuna mambo mbalimbali yameanza kujitokeza katika jamii kama mavazi yasiyozingatia maadili ambayo si utamaduni wa Kitanzania na kwamba mambo hayo yanachangia ushawishi wa ngono zembe na kuongezeka kwa maambukizo ya Ukimwi.
“Ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda amani na utulivu huo ili nchi yetu iendelee kutukuka kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu japo wapo baadhi ya watu wameanza kutaka kuharibu sifa hiyo.”
Songea
Sheikh wa Msikiti wa Wilaya ya Songea, Ruvuma, Abdallah Kitete amesema kuna kila sababu ya waumini na wanasiasa kuhubiri amani kwani pasipo vitu hivyo hakuna utawala...”Huwezi kutawala watu sehemu ambayo haina amani....”

Aliitaka jamii ijitahidi kuiga mwenendo wa Mtume Muhammad (SAW), alivyoishi na watu wa dini zote bila kuwabagua huku akiwa mstari wa mbele kuhubiri upendo, amani na mshikamano na ndiyo maana dini yake ilienea dunia nzima.

KWA HABARI ZAIDI====>BOFYA HAPA