Showing posts with label TECHNOLOGY. Show all posts
Showing posts with label TECHNOLOGY. Show all posts

TIPS | Jinsi ya Kuhifadhi na Kutumia Mfumo wa Android kwenye Kompyuta Yako

Android ni moja ya mfumo maarufu zaidi duniani wa kuongoza simu, ikiwa imeunganisha kampuni nyingi na kubwa sana za kutengeneza simu janja.

Simu janja kutoka Samsung, Sony, HTC, Huawei, Tecno, sasa hata baadhi ya Nokia au Blackberry zinatumia mfumo huu, japo kwa matoleo tofauti kulingana na uwezo wa simu..

Lakini ukubwa wa mfumo huu wa simu janja duniani, hakujazuia mfumo huu kuweza kuwekwa na kutumiwa katika Kompyuta za kawaida. Kuna namna tofauti za kutumia mfumo huu kwenye kompyuta, kama kutumia Kifaa Maalum Cha mfumo wa Android kwenye kompyuta yako, Kuweka mfumo wa uendeshaji (OS) wa adroid kwenye kompyuta yako au kutumia App maalum..

Hii ina maana kuwa, ukiwa na mfumo wa Android kwenye PC yako, utakuwa na uwezo wa ‘Kuinstall’ na kutumia App na Game zote zinazopatikana kwenye Playstore katika PC yako. Ndio. Tuangalie Njia moja baada ya nyingine upate maujanja zaid...


Kwa Kutumia App kama Vile BlueStacks

Njia hii ndio rahisi, na yenye faida zaidi kwa watumiaji wa kawaida.  Kutumia app kuendesha mfumo wa android kwenye PC yako ni rahisi kwa sababu unahusisha Mfumo wako unaotumia kwa wakati huo (Windows 7, 8, 8.1, au 10). App kubwa na inayofanya kazi vizuri zaidi ni BlueStack.

Ilianzishwa mwaka 2011 kwa ajili ya kuunganisha mfumo wa android kwenye PC yako. Ukiwa na BlueStack, mtumiaji unaweza kudownload App na Games mbalimbali kutoka PlayStore, au Amazon AppStore kusha kutumia App hizo katika PC yako..

BlueStack imerahisishwa sana kwa watumiaji, kwani unaweza kuinstall na kufanya mipangilio inayofanana kabisa na ile ya Simu janja yako. Picha kutoka Android Authority...


 Ukishusha mfumo wa BlueStack, utapata Toleo la 4.4.2 KitKat la Android. Japo ni matoleo mawili nyuma ya mfumo wa sasa, lakini kuna dalili za kuletwa Masasisho ya App hii maarufu sasa kwa watumiaji wa PC.

Japo ina kasoro zake, mfano kucheza baadhi ya michezo ya 3D, au baadhi ya michezo ya 1080p kwa kushindwa kuchezesha vivuli n.k. Lakini watumiaji wanafurahia huduma nyingine muhimu za App kama Whatsaap, Instagram na Games. Vyote vilivyo PlaStore. BlueStack pia inakuwezesha kuhamisha mafaili kama yale ya APK kutoka kwenye komputa kwenda kwenye simu ya Android.

Ni mfumo mzuri, na mrahisi kutumia kama ni mara ya kwanza kuanza ujanja huu. Unaweza ukaudownload kwenye PC yako kwa kubonyeza HAPA 


TIPS | Jinsi Ya Kufufua Mafaili Yaliyofutwa Katika Simu/Kompyuta


Ikiwa kwa makusudi au hata bahati mbaya umefuta data zako katika memori kadi ya simu yako, ‘hard drive’ au kifaa kingine, na baadae ukawa unazitaka tena, je unaweza zipata? Ndio unaweza zipata!. Unaweza pata tena data zako ulizofuta katika SD Card / Hard Disk Drive kwa msaada wa Asoftech software.

Asoftech ni programu ya kuzifufua data zilizofutwa ambayo ni ya bure kushusha na rahisi kutumia na pia ina ukubwa mdogo  (kama 4MB hivi) kwa msaada wa hii programu (software) utafufua mafaili yaliyofutwa kwenye vifaa vya uhifadhi wa data mbalimbali kama vile ‘pen drive, USB drive, external Hard Drive, memory card’ na sehemu zingine

Inabidi kuacha kutumia mafaili katika simu yako mara tuu unapotaka kufufua mafaili yaliyofutika katika SD Card  kwa sababu haitawezekana kufufua mafaili wakati mafaili mengine yanatumika muda huohuo katika simu.

Kitu kingine cha kuweka akilini ni kwamba hautawezekana kufufua mafaili kwa kutumia Asoftech kama utakua umefomati (Format) SD Card/Hard Drive  ya kifaa chako

FUATA NJIA HIZI KUFUFUA MAFAILI HAYO...

 1. Kwanza kabisa inabidi uishushe hiyo programu (Software) ya Asoftech HAPA

2. Baada ya kuishusha (download) fanya mpango wa kuipakua (install)….. itakuchukua muda kidogo tuu

3. Kutumia Asoftech inakubidi uwe ‘Administrator’ katika kompyuta yako, kama ni Admin nenda mpaka kwenye icon ya Asoftech ‘ Right Click’ kisha bofya ‘Run As Administrator‘.