FAIDA ZA KULA NYANYA

.

Nyanya huwa tunazichukuliwa kama mboga za majani, ingawa ni kiuhalisia ni tunda.
Nyanya ni chakula kizuri sana. Ni tamu ukila mbichi katika kachumbari au katika sandwiches, na zinakuwa na utamu wa aina yake zikiwa zimepikwa.

Nyanya chakula muhimu sana katika mlo wa watu wa Africa hususan hapa kwetu Tanzania Nyanya moja inakuwa na calorie 22, gramu 0 za mafuta, gramu 5 za wanga, gramu 1 za fiber, gramu 1 ya protini na miligramu 6 za sodium. Pia inatoa asilimia 40 ya vitamin C inayoshauriwa kula kwa siku, asilimia 20ya vitamin A, asilimia 2 ya chumba,  na asilimia moja ya calcium.

Zifuatazo ni faida za nyanya:
1.Kinga dhidi ya Saratani.
Tafiti mbalimbali zithibitisha kadiri watu wanavyokula nyanya nyingi ndivyo inasaidia kupunguza uwezekano wakupata saratani za mapafu, tumbo na kizazi. Kitu kinaitwa lycopene kinachofanya nyanya ionekane nyekundu kwa rangi inadhaniwa kuwa ndio sababu inanyoifanyanyanya iwe na uwezo huowa kinga.

Nyanya zilizopikwa ndio zina lycopene nyingi kuliko nyanya mbichi.
Mchakato wa kuzipika nyanya zinavunja vunja kuta za chembechembe hai ambako kunasaidia kutoka kwa lycopene. Ukila nyanya kwa vitu vyenye mafuta kama mafuta ya olive inasaidia lycopene kuingia vizuri mwilini.

2. Zinalinda Dhidi ya uharibifu wa DNA.
Nyanya uwingi wa antioxidants kama Vitamini C na Vitamin A. Vitamini hizi zinafanya kazi ya kulinda DNA dhidi ya kuharibiwa. Pia nyanya zinaweza kukusaidia kukukinga dhidi ya magonjwa yanakupata uzeeni kama kisukari.

3. Inapunguza Hatari Ya Ugonjwa Wa Moyo.
Nyanya zina virutubisho muhimu kama niacin, folate na vitamin B6 ambazo zinahusika na kupunguza uwezekano wakupata ugonjwa wa moyo.
Utafiti mmoja uligundua kuwa wanawake waliokula nyanya saba mpaka kwa wiki walikuwa na asilimia 29 pungufu za kupata ugonjwa wa moyo  ukilinganisha na wanawake waliokula pungufu.
Matokeo ya utafiti huu yalikuwa mazuri zaidi kwa wale wanawake waliokula nyanya na vyakula vyenye mafuta.

4. Zinakulinda dhidi ya thrombosis.
Thrombosis ni kuganda kwa damu katika mishipa (blood clots in the blood vessel). Utafiti unaonyesha kuwa ni muhimu kula nyanya zenye sodium kidogo kama unataka kujikinga dhidi ya thrombosis.

5. Kuzuia Kuvimba.
Utafiti unaonyesha kuwa kunywa glasi moja ya nyanya kwa siku kunasaidia kupunguza TNF-alpha kwa asilimia 34 katika damu. TNF-alpha inasababisha kuvimba mwili.
TNF-alpha nyingi hupatikana kwa watu wenye magonjwa sugu kama ugonjwa wa moyo, saratani, osteoporosis na Alzheimer’s.
Kula nyanya nyingi iwezekanavyo ilikupata afya njema.

Kwan nchi yetu ya Tanzania upatikanaji wa nyanya ni rahisi sana tena itakuwa vizuri kama katika kila mlo wako wa siku utakuwa unatengeneza kachumbari yenye mchanganyiko wenye nyanya nyingi.

Endelea kuwa na Afya Njema.