IJUE THAMANI YA KICHWA CHA SAMAKI-unaweza kipika hivi….

Supu/mchuzi wa Kichwa cha Sangara.

Moja kati ya mambo ninayoyapenda sana kuhusu my home town MWANZA  A.K.A. THE ROCK CITY ni Samaki.Samaki wanaopatikana ziwa Victoria wana sifa kubwa  sana kitaifa na kimataifa.

Ukiishi mikoa yakanda ya ziwa huwezi jua thamani ya samaki hao adi utoke nje ya mkoa uwakose kwa muda.Samaki wa maji baridi si kama wa maji chumvi,wanatofautiana ladha na zaidi ya yote wanatofautiana ainana wingi wa virutubisho.

Samaki  kwa ujumla ni chanzo kikubwa cha protini na madini mwili,samaki wa maji baridi wana Omega -3 na fatty acids kidogo ukilinganisha na samaki wa maji chumvi,ata ivyo samaki wa maji baridi ana protini nyingi na mafuta kidogo,pia anamadini mwili kama  calcium,madini chuma pamoja na manganese.

Samaki hutumika kama kitoweo kwachakula cha mchana na jioni kwa familia nyingi.Kwa wakazi wa maeneo ya ziwani samaki huliwa ataasubuhi kama kifungua kinywa kwani hupatikana kwa wingi katika maeneo hayo.Kichwa cha sangara kina sifa ya kutoa supu au mchuzi mzito,kina mafuta na kwa ujumla ni kitamu.

Kwa miaka mingi kumekua na imani iliyojengeka kwenye makabila ya kanda ya ziwa kwamba ukila kichwa cha samaki unakua na akili nyingi.Watu wengi sana hawakubaliani na imani hii ata kidogo na mara nyingi nimesikia watu wakiongelea vibaya au kutania juu ya imani hii.

Ukweli ni kwamba,imani yao ni ya kweli na inathibitika kisayansi.kichwa cha samaki hubeba asilimia kubwa ya madini na  mafuta mengi kuliko sehem yoyote ya samaki ,mafuta hayo hubeba  essential Fatty acids(Omega -3 na omega-6) na  madini mwili aina ya calcium,madini chuma,manganese.

Madini haya pamoja na assential fatty acids ni virutubisho muhim sana katika ujenzi na ukuaji kwa ubongo.kila kirutubisho kina  kazi yake maalum.Hivyo kwakua wakazi wa kanda ya ziwa hupata virutubisho hivyo kwa wingi basi ubongo wao hukua vizuri na kuwapa uwezo wa kua na akili zaidi.

Ni vyema kujua kwamba ukuaji wa Ubongo wa mtoto huwa katika kiwango cha juu kabisa ndani ya miaka miwili ya kwanza ya maisha ya mtoto,hata ivyo virutubisho hivi na vingine vingi huendelea kua muhim katika utendaji na ukuaji wakilasiku wa ubongo.

Kwa upande mwingine Akili hukua na kuongezeka sawasawa na akuavyo mtoto.kumbuka tu,endapo ubongo wake ulikua vizuri na unapata virutubisho muhim ili kuuwezesha kufanya kazi vizuri  basi akili yake huwa na uwezo wa kukua na kupanuka kwa haraka zaidi.niishie hapa nisijeingilia fani ya madaktari Nilipokwenda Mwanza kwa ajili ya christmass mwaka jana,sikufanya kosa,nilikula samaki kwa wingi,na nilianda,nikapika  na kula kichwa cha sangara kwa hamu sana.

Kuna namna na njia nyingi za kupika na kuanda kichwa cha samaki,na hii ni namna moja wapo.

Vipande vya sangara tayari kwa kupika.

Mahitaji:
*.Kichwa cha sangara.kipasue vipande
*.Maji
*.Nyanya
*.Kitunguu maji
*.Kitunguu swaumu
*.Limao au ndimu
*.chumvi

Njia.
1.Osha kichwa cha sangara vizuri,zingatia sana mashavu kwani hubeba uchafu mwingi

2.Weka samaki  ndani ya sufuria zito,kisha ongeza maji adi yafunike samaki na kuzidi kidogo.

3.kisha ongeza vitunguu maji,vitunguu swaumu,nyanya na chumvi kisha bandika jikoni vichemke kwa muda mrefu na kwa moto wa wastani.moto ukiwa mkali hutapata mchuzi au supu nzuri na wakati kinatokota kichwa kitameguka meguka.

4.Chemsha adi kiive,kisha ongeza limao kabla tu ya kuepua .kama ni kwa ajili ya mtoto usiongeze limao,ila mpe juice ya chungwa  baada ya kula mlo wenye samaki.Wingi wa supu au mchuzi ni chaguo la mpishi,kama unataka supu/mchuzi mwepesi  basi hakikisha umeweka maji mengi zaidi unapoanza kuchemsha,ni vyema upima maji ya kutosha unapoanza kuchemsha ili uepuke kuongeza maji baada ya kuchemka,maji ya nyongeza siku zote huaribu ladha na ubora wa supu na hata mchuzi.

Mambo ndio kama hivyo,Kichwa chasangara tayari kwa kula,unaweza ukanywa supu yake na kula kichwa bila kusindikiza na chakula kingine,na ukipenda unaweza kutumia kama mboga au kitoweo.

IPE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA SI BORA CHAKULA.