AFYA | FAHAMU UKWELI KUHUSU ALOEVERA...

 FAHAMU UKWELI KUHUSU ALOVERA.

UTANGULIZI:
Matumizi ya mimea ya asili yamekuwa yakitumika miaka zaidi ya elfu tatu kabla Kristo(3000BC) , Kila kabila na taifa limekuwa likitumia mimea mbalimbali kwa ajili ya kujitibu na kuboresha afya. Inakadiriwa takribani 75% ya watu duniani wanatumia mitishamba kwa ajili ya kujitibu.
Utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa ili kuzuia maradhi unapaswa;


1.Mwili uwe unapata viini lishe vya aina sita(Basic Essential Nutritional Supplements), vikiwemo amino acids 8 muhimu, vitamins 18 muhimu na madini 20, kutoka kwenye mitishamba,matunda, bidhaa za nyuki na mafuta mazuri kama yatokanayo na samaki aina ya salmon n mzaituni.
2.Mwili inabidi upate hewa ya OXYGEN, MAZOEZI ya mara kwa mara na Kunywa MAJI ya kutosha.
Kumbuka mwili utajiponya wenyewe kama tuu utafuata taratibu muhimu za kuupa chakula kamilifu, kuufanyisha kazi na kuupumzisha vizuri. Tukumbuke vyakula tunavyokula vinapungukiwa na viinilishe na vingine vina sumu nyingi hivyo huharibu mwili.

UKWELI KUHUSU ALOEVERA
Aloe vera ni mmoja kati ya mimea iliyojulikana tangu kitambo sana.Una zaidi ya miaka 2000 katika historian a sayansi. Kuna zaidi ya aina 200 za mimie ya aloevera(shubiri), una zaidi ya virutubisho 75 vikiwa ni pamoja na madini 20, amino acid 18 na vitamins 12.

Aloevera(Shubiri) ina faida kuu tano kwa mwili wa binadamu kama ifuatavyo:
1.Huua vimelea vya magonjwa-ina vichocheo sita vinavyoua vimelea vya magonjwa kama bacteria, virusi na fangasi.
2.Uzalishaji wa chembe hai za mwili-huchochea utengenezwaji wa chembechembe mpya na tishu mpya zenye afya.

3.Hufanya mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri-Hutuliza matatizo yanayoathiri mfumo wa fahamu.
4.Husafisha-Huondoa sumu mwilini na kufanya utendaji kazi wake urudi katika hali ya kawaida, pia hupunuguza alegi mwilini
5.Aloevera ni kinywaji cha asili ambacho huboresha na kuondoa maradhi mengi katika miili yetu.

ALEOVERA INAWEZA KUSAIDIA KATIKA MAMBO YAFUATAYO:
1.Vidonda vitokanavyo na kuungua, kujikata, michubuko, vidonda vya tumbo, kung’atwa na wadudu wakali na wanyama.
2.Matatizo ya kutopata haja hasa maumivu wakati wa kupata haja kubwa.
3.Matatizo ya ngozi psoriasis, pumu ya ngozi(eczema), chunusi(acne) na dermatitis.
4.Shida ya mmeng’enyo wa chakula,ugonjwa wa koo, pumu na uchovu wa mwili usioeleweka.
5.Aloevera ni salama haina madhara kwa binadamu, kimsingi ni kama juisi, Hata ukizidisha kipimo haileti madhara.Inaweza kutumika ndani ya mwili kwa kunywa au nje ya mwili kwa kupaka.

UFANYAJI KAZI WA ALOEVERA NDANI YA MWILI
Utafiti unaonyesha kwamba 90% ya magonjwa yote huanzia kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kwa hiyo mmeng’enyo mzuri wa chakula, unyonywaji na usafirishaji wa virutubisho ni muhimu kwa afya bora.
Sumu na mafuta huziba ukuta wa sehemu ya utumbo iitwayo vilai, na kuzuia ufyonzwaji wa viini lishe na vitamin vinapita na kutoka nje kama uchafu bila kufyonzwa. Wakati mwili unakosa virutubisho kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mwili hupata upungufu na kusababisha magonjwa mbalimbali. Unapokunywa aloevera unasidia kuondoa sumu kutoka kwenye mfumo wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusadia ufyonzwaji wa viini lishe na vitamin zilizopo kwenye vyakula tulavyo. Kwa kuwa miili yetu kwa muda mrefu imekuwa na sumu, hivyo ndio sababu unashauriwa kutumia aloevera na virutubisho vingine ili kusaidia mwili kurekebisha mfumo wake kwa ujumla.