AFYA | ZIJUE SABABU KWA NINI UTUMIE MAFUTA YA SAMAKI...

  ZIJUE SABABU 4 ZA KWA NINI UTUMIE MAFUTA YA SAMAKI.

Utafiti ulifanywa kwa nini wajapani hawaugui magonjwa ya kansa,kisukari na magonjwa ya moyo, ikaonekana kwamba wajapani wanatumia sana vyakula vya baharini ukilinganisha na watu wa magharibi wanaotumia mafuta na nyama.
Ukweli ni kwamba mafuta ya samaki yana omega 3 ambayo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu.



Zifuatazo ni faida za kutumia mafuta ya samaki(omega 3);
1.AFYA YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU.
Mafuta ya samaki yenye omega 3 yanasaidia kupambana na tatizo la cholestral ambayo ni mafuta mabaya yaliyoganda katika mishipa ya damu. Cholestral husababisha matatizo kama shinikizo la damu, kiharusi na mengine mengi.
2.UKUAJI WA UBONGO NA KUTUNZA KUMBUKUMBU.
25% ya mafuta yanayotakana na samaki ni muhimu kwa kwa afya ya ubongo na utunzaji kumbukumbu. Mafuta haya pia ni muhimu kwa watoto kwani yanaongeza uwezo wao kiakili(intelligence), uwezo wa kutunza kukumbuka. Mtu anayetumia mafuta ya samaki ni vigumu kupatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu(Alzheimer’s disease).
Mama mjamzito anashauriwa kutumia mafuta ya samaki kabla,wakati na baada ya kujifungua kwa ajili ya kumsaidia mototo aliyeko tumboni kwa kupata faida tajwa hapo juu.
3.KUONGEZA UWEZO WA KUONA
Mafuta haya yanasaidia kuongeza uwezo wa macho kuona vizuri na kupambana na matatizo mengine yanayoathiri macho kuona vizuri.
4.KUPUNGUZA KASI YA UZEE
Mafuta ya samaki yanasaidia mwili kuongeza uwezo wa kutumia vizuri chakula(metabolism), yanaongeza afya ya mfumo wa mzunguko wa damu, yanalinda ngozi na miale mibaya ya jua(ultra-violet rays) hivyo kuwezesha mwili kupambana na hali ya uzee.
Ubora wa mafuta ya samaki ni jambo lingine la msingi la kuzingatia. Mafuta ya samaki yanayotokana na samaki wa maji safi na wanaovuliwa maeneo yasiyo na uchafuzi ni bora na yana thamani kuliko yale ya samaki waliovuliwa katika bahari yenye uchafuzi.
Ikiwa unahitaji mafuta ya samaki(omega 3) yenye ubora wa kimataifa,