FAIDA YA KITUNGUU NA JUISI YAKE


Kitu kimoja napenda kukuhakikishia kuwa, unayoyasoma hapa kuhusu kitunguu, tayari yalishafanyiwa utatifi na kuthibitishwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya vyakula tangu enzi za mababu zetu. Vile vile, watu wanaoamini lishe kama tiba na kutumia, matokeo yake siku zote huwa dhahiri na wako wengi wanaoweza kuthibitisha jinsi afya zao zilivyo imara leo tofauti na miaka kadhaa iliyopita kabla ya kugundua siriya chakula kama tiba.




JINSI YA KUTENGENEZA...


Kinachotakiwa ni kitunguu maji kimojacha ukubwa wa wastani ambacho utatengenezea juisi na kupata kiasi chaglasi moja saizi ya kati. Safisha kitunguu chako kwa kuondoa gamba lajuu kisha katakata vipande vidogo vidogo ili kurahisisha usagaji. Kuna njia mbili unazoweza kuzitumia kutengeneza juisi hiyo.




Ya kwanza ni ya kisasa ambapo unaweza kutumia 'blender' au 'juicer', kwa kuweka maji kidogo na kuanza kuisaga hadi kupata juisi.




Njia ya pili ni ya kiasili, ambapo utatumia kinu kidogo na maji kidogo kwa kutwangwa hadi kupata juisi. Ukimaliza kusaga (kwa njia utakayoitumia) kamua na ichuje juisi yako kwa kutumia chujio la kawaida ili kupata juisi pekee ya kitunguu na kuacha masalia ya maganda peke yake.


Mara baada ya kuiweka juisi yako kwenye glasi, HAKIKISHA UNAINYWA HAPO HAPO. Hairuhusiwi kuihifadhi au kuinywa baadaye, kwa sababu itapoteza virutubisho vyake muhimu. Kunywa glasi moja mara moja kwa sikuau mara mbili, ukiona tatizo lako ni kubwa. Fanya zoezi hilo la kundaa juisi na kuinywa kwa muda wa siku saba hadi 14.


Kama nilivyoeleza wiki jana, hali ya kuchafuka kwa tumbo na kujisikia vibaya baada ya kunywa, isikuogopeshe, baadaye utaizoea na utajisikia vizuri zaidi. Mbali ya kutibu tatizo la kusikia maumivu na kutokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa (Hemorrhoids au piles), juisi hiyo pia itatoa ahueni aukinga kubwa dhidi ya matatizo mengine ya kiafya yafuatayo: Pumu, mafua, magonjwa ya kuambukizwa na bakteria, matatizo ya kupumua kwa shida, kiungulia na kutapika. Itaongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi, vile vile kwa kutafuna vitunguu vibichi na kukaanavyo mdomoni kwa sekunde kadhaa, kutaua bakteria wote wa kinywani na kutoa kinga dhidi ya kuoza kwa meno na kuondoa harufu mbaya. Ulaji wa vitunguu maji vibichi mara kwa mara, hulainisha damu na kuzuia kuganda ambako husababisha mishipa kuziba na kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwemo presha ya kupanda.


Juisi ya kitunguu ni dawa mara moja yakuzuia kutapika, mtu anayetapika mfululizo akinywa juisi ya kitunguu, hupata nafuu haraka. Vile vile juisi hii ni dawa ya tumbo linalouma na hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe tumboni. Kama unasumbuliwa na chunusi, pakaajuisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali sehemu yenye chunusi vitaondokana kukuacha na ngozi nyororo. Chukua kiasi kidogo cha juisi na kijiko kimoja kidogo cha asali changanya kisha pakaa. Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyuki. Kama unapata maumivu wakati wa haja ndogo au unatoa mkojo mchafu sana, kunywa maji mengi yaliyochanganywa na juisi ya kitunguu kiasi kidogo, tatizolitakwisha. Juisi ya kitunguu ina virutubisho vyenye uwezo wa kudhibiti chembechembe hai za mwili zenye kansa na hivyo kuwa kinga nzuri dhidi ya ugonjwa wa saratani (cancer). Ulaji wa vitunguu au juisi pia hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kifua kikuu.


Juisi iliyopashwa moto pia ni dawa ya sikio linalouma. Weka matone mawili tu kwa kila sikio linalouma. Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya majeraha yatokanayo na moto. Ukiungua, pakaa juisi hiyo sehemu zilozoungua kwa nafuu ya haraka. Pia kitunguu ni dawa ya mbu, pondapondavitunguu, kisha jipakae sehemu za miguu na mikono - mbu hawatakugusa. Faida za kitunguu na juisi yake ziko nyingi na zote ni muhimu kwa ustawi wa afya zetu. Nakushauri kuanzia leo, kunywa juisi hiyo au kula kitunguu katika kila mlo kwa jili ya kutibu maradhi uliyonayo au kwa kuupa mwiliwako kinga imara, na kamwe hutajuta!